January 19, 2014


Mshambuliaji Mcameroon, Samuel Eto’o maarufu kama Shemeji hapa nchini ameweka rekodi mpya ya kufunga mabao matatu.


Chelsea imeichapa Man United kwa mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu England iliyopigwa Uwanja wa Stamford Bridge jijini London.

Bao la ‘kufutia’ hasira la Man United lilifungwa na Chicharito aliyeingia kipindi cha pili.

Eto'o ambaye baadhi ya wachambuzi wamekuwa wakisema amekwisha au kumalizika kabisa kwa kiwango chake alionekana mwiba kwa mabeki wa United.

Man United walionekana hatari katika dakika saba za mwanzo, baada ya hapo wakapoteza uelekeo.

Kama Chelsea wangekuwa makini zaidi wangeweza kushinda zaidi ya mabao hayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic