January 19, 2014





Sehemu mbalimbali kwenye mitando suala la gari aina E-Vogue ambalo limeelezwa kuwa jipya la Lady Jaydee limezua gumzo sana.

Msanii huyo mkongwe ameonekana amepiga pozi nyuma ya gari hilo ambalo limeelezwa kuwa analimiki.
 
KIFAA CHA E VOGUE
Ingawa Jaydee mwenyewe bado hajasema lolote kuhusiana na gari hilo, lakini mashabiki wengi wa muziki wamejitokeza kumpongeza.
Kulingana na aina, Range Rover E-Vogue ambayo asili yake nchini Uingereza unaweza kulipata kwa kitita cha kuanzia Sh milioni 50 hadi 120 milioni.
E-VOGUE KWA NDANI, UTAFIKIRI NDEGE BANA!
Gari la kwanza la Jaydee mwanzoni mwa miaka ya 1990 lilikuwa ni Suzuki Vitara la milango mitatu lakini mwadada huyo amekuwa akiendelea kubadilisha magari aina tofauti kadiri siku zinavyosonga kwenye muziki.
Baadhi ya magari ni kama Toyota Prado ya aina tofauti, moja alipata nalo ajali mumewe G Habash likaharibika vibaya lakini baadaye akanunua Nissan Murano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic