MILOVAN NA MWENZAKE WAKIWA WAMESHIKA JEZI ZA MYNMAR |
Kocha wa zamani wa Simba, Milovan
Cirkovic ameula baada ya kupata ajira mpya ya kocha msaidizi wa timu ya taifa
ya Myanmar.
HUYU NDIYE BOSI WA MILOVAN |
Milovan amethibitisha kuingia mkataba wa
mwaka mmoja na nusu katika nafasi hiyo na tayari yuko nchini humo.
Kocha huyo wa zamani wa Simba atakuwa
chini ya kocha mwingine mzoefu, Raddy Avramovic ambaye
aliwahi kuwa kocha mkuu wa Singapore mwenye mafanikio makubwa.
Jana kulikuwa na sherehe maalum
iliyofanywa na Shirikisho la Soka la Myanmar (MFF) kuwakaribisha makocha wote
na benchi zima la ufundi akiwemo Milovan.
“Kweli sasa niko hapa na mambo
yamekwenda vizuri, kazi yetu ndivyo ilivyo ni safari kila siku, ila ninafurahi
kuwa hapa,” alisema Milovan katika mahojiano na SALEHJEMBE.
0 COMMENTS:
Post a Comment