March 9, 2014


Mechi kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly imemalizika
Mabingwa hao wa Afrika wametokea kwenye tundu la sindano baada ya kupata ushindi wa penati 4-3.

Katika dakika 90, Ahly walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa katika dakika ya 70.
Katika mikwaju ya penati, Mabeki Mbuyu Twite na Oscar Joshua walikosa baada ya penalti zao kupanguliwa.

Kipa Deo Munishi alirekebisha mambo baada ya kupangua penalti 2. Ilikuwa ni zamu ya Said Bahanuzi ambaye kama angefunga, basi Yanga ingefuzu.
Lakini mkwaju aliopiga ulitoka nje na baada ya hapo, Ahly wakamalizia penati ana kufuzu kwenye hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic