March 11, 2014

NGASSA AKIWA NJE WAKATI WENZAKE WAKIJIFUA LEO. ANAYEFUATIA NI MSEMAJI WA YANGA, BARAKA KIZUGUTO NA DAKTARI, JUMA SUFIANI.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa ameendelea kukaa nje bila ya kufanya mazoezi kutokana na daktari wa timu hiyo kuona hayuko fiti.

Daktari wa Yanga, Juma Sufiani amesema bado hajawa katika kiwango cha kujumuika na wenzake baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Al Ahly.

“Bado hajawa katika hali nzuri, sasa anaendelea na matibabu, hivyo naweza kusema bado hajawa fiti,” alisema.

Ngassa alitolewa wakati wa mechi hiyo juzi kwenye Uwanja wa Max jijini Alexandria baada ya kuumia.


Katika mechi hiyo, Yanga ililala kwa mikwaju ya penalty 4-3 na kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic