MADADI |
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limemteua Salum Madadi kuwa Mkurugenzi wake
mpya wa Ufundi.
Uteuzi
huo umefanya na Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha dharura
kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Kabla
ya uteuzi, Madadi alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Januari mwaka huu baada ya
Mkurugenzi wa Ufundi aliyekuwepo kumaliza mkataba wake Desemba 31 mwaka jana.
Madadi
mwenye leseni A ya ukocha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni kocha
mwenye uzoezi wa zaidi ya miaka 30 ambapo alianza kufundisha mpira wa miguu
mwaka 1980 katika klabu ya Maji SC ya Lindi.
Ana
elimu ya sekondari aliyoipata katika shule ya Chidya na diploma ya ukocha wa
mpira wa miguu aliyoipata nchini Ujerumani. Pia ni Mkufunzi wa makocha wa CAF,
na alijiunga na TFF mwaka 2006 akiwa Ofisa Maendeleo.
Alikuwa
Kocha wa Taifa Stars mwaka 2000. Mbali ya Maji SC, amewahi kufundisha timu za
Nyota Nyekundu, Ushirika ya Moshi, Simba, Shangani ya Zanzibar, Malindi ya
Zanzibar, Cardif ya Mtwara na Kariakoo ya Lindi.
Pia
amewahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu
Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
0 COMMENTS:
Post a Comment