March 29, 2014



Kocha Jose Mourinho amesema alimvaa Kocha Jose Mourinho kwa kuwa aliamua kumshauri kama kijana wake.

Mourinho alisema aliamini kijana huyo muokota mipira alikuwa akifanya kitu ambacho si sahihi, kama mzazi alipaswa kumueleza.
“Ilikuwa ni lazima kutoa mafunzo, mimi ni mzazi na kama kijana anafanya tofauti na kawaida, basi ni muhimu kumueleza jambo,” alisema.

Mourinho alimfuata kijana huyo kwa kasi wakati alipochelewesha mpira, akainama na kuanza kumnong’oneza, hata hivyo hakusema alimueleza nini ingawa baada ya kuzungumza naye, mtoto huyo alionyesha kutikisa kichwa kama alielewa kitu fulani.

Chelsea ambayo inachuana na Liverpool, Man City na Arsenal kuwania ubingwa England, ilitibua mambo baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic