March 30, 2014



Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema haitakuwa kazi lahisi kwa kikosi chake katika mechi ya leo dhidi ya Azam FC, lakini akasisitiza anahitaji ushindi.

Logarusic amesema Simba ina uwezo wa kuifunga Azam FC ingawa anaamini ni moja ya timu ngumu zaidi kwenye  Ligi Kuu Bara.
“Itakuwa mechi ngumu na kutakuwa na mapambano ya kweli, lakini ninataka ushindi na tuna uwezo wa kufanya hivyo,” alisema.
“Kama wachezaji watafuata maelekezo, basi hakuna cha kutuzuia kushinda. Tuna kiwango cha kufanya hivyo hata kama tunapambana na timu bora.”
Azam FC watakuwa wenyeji wa SImba katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic