March 31, 2014


Ushindani wa timu moja itakayopanda daraja hadi Ligi Kuu Bara kutoka kundi C umebaki kwa timu mbili za Mwadui na Stand United, zote za mkoani Shinyanga baada ya Toto Africans kufungwa juzi Jumamosi.

Lakini sasa hakuna ubishi kuwa mkoa wa Shinyanga tayari umepata timu itakayoshiriki Ligi Kuu.

Stendi na Mwadui zote zinatokea mkoani humo na Mwadui inanolewa na kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio'.


Mwadui waliwachapa bao 1-0 na kufikisha pointi 28, Stand ikaifunga Kanembwa JKT 3-2 na kufikisha pointi 26. Mechi za mwisho zitakazochezwa wikiendi ijayo, ndizo zitakazotoa jibu kamili la timu itakayoungana na Polisi Moro na Ndanda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic