April 2, 2014


Nahodha  wa Azam, John Bocco ‘Adebayor’, amefunguka kuwa, hakuna timu yoyote itakayoweza kuwaondoa katika nafasi ya kwanza msimu huu.


Azam ilijiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba, Jumapili iliyopita.

Ushindi huu umewafanya Azam wakae kileleni zaidi wakiwa na pointi 53 zikiwa ni saba mbele ya Yanga inayoshika nafasi ya pili.

Bocco amesema wanacheza kwa kujituma ili waweze kuchukua ubingwa  msimu huu na hatua waliyofikia hakuna wa kuwazuia.
“Tunacheza  kwa kujituma ili tuzidi kuwa juu, ushindani uliopo ni mkubwa, sasa tunachokifanya ni kuhakikisha tunashinda michezo yote ili tuchukue ubingwa ambao kila mchezaji anautaka.


 “Tumebakiwa na mechi ngumu ambazo tunakwenda kucheza ugenini, lakini tutafanya juu chini tuibuke na ushindi katika mechi zote zilizobaki,” alisema Bocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic