Wachezaji wazoefu wa Taifa Stars
watakaoungana na wale 16 waliopatikana katika mpango wa maboresho wa timu hiyo
watatangazwa kesho (Aprili 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itapiga kambi kwenye hoteli ya Kunduchi Beach
kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka
huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji waliopatikana katika mpango
wa maboresho ya Stars wanatarajiwa kuwasili leo (Aprili 18 mwaka huu), na
kwenda moja kwa moja kambini kuwasubiri wenzao watakaotajwa kesho (Aprili 19
mwaka huu).
Wachezaji hao ni kipa Benedicto
Tinoko Simwanda (Mara), Emma Namwondo Simwanda (Temeke), Joram Nason Mgeveje
(Iringa), Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba),
Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala), Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke) na Said Juma
Ally (Mjini Magharibi).
Wengine ni Abubakar Ally Mohamed
(Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje
(Mtwara), Chunga Said Zito (Manyara), Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini
Magharibi) na Paul Michael Bundara (Ilala).
0 COMMENTS:
Post a Comment