ALIYEKUWA kipa wa Simba, Mganda, Abel Dhaira (26), anayechezea IB
Vestmsnnseryjav ya nchini Iceland kwa sasa, ametua nchini Hispania kwa ajili ya
kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Daraja la Kwanza nchini humo.
Dhaira alijiunga na Simba msimu uliopita na kucheza mzunguko wa
kwanza kabla ya kutemwa kutokana na kuonyesha kiwango kidogo kwenye ligi.
Akizungumza na gazeti hili, kipa huyo alisema timu yake kwa sasa
imehamishia kambi Hispania kutokana na baridi kuzidi nchini Iceland na sasa
wanajiandaa vyema kwa ajili ya ligi hiyo.
Dhaira alisema timu yake hiyo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza na
amefanikiwa kupata namba katika kikosi cha kwanza na maendeleo yake ni mazuri
na anaendelea kuongeza bidii zaidi ili atimize ndoto zake za kuwa mchezaji
bora.
“Tupo nchini Hispania ambapo tumeweka kambi huku kutokana na
kipindi hiki kuwa na baridi kali Iceland, tunashukuru tunaendelea vizuri na
maandalizi na lengo letu ni kuhakikisha tunafanya vizuri.
“Lakini kitu muhimu kwangu kwa sasa ni kwamba nimepata namba
katika kikosi cha kwanza na naendelea vizuri na timu ipo katika nafasi nzuri
kwenye ligi,” alisema Dhaira.
0 COMMENTS:
Post a Comment