April 2, 2014


Kocha Mkuu wa Ndanda FC ya mkoani Mtwara, Denis Kitambi, amefunguka kuwa wanahitaji wachezaji saba kuongeza nguvu msimu ujao.


Ndanda imepanda daraja kwa ajili ya kucheza ligi kuu katika msimu wa 2014/2015 na tayari mashabiki wameshaanza kuiunga mkono.

Kitambi amefunguka kuwa wanahitaji wachezaji wenye uwezo ili kufanikiwa kuleta ushindani kwenye ligi msimu ujao.
“Tunatarajia kuongeza mtu mmoja-mmoja katika kila idara ili kuongeza nguvu msimu ujao na kuleta ushindani.

“Hatujajua usajili utakuwaje hadi uongozi utakapokutana na kuweka kikao cha kufanya tathmini ili kupata kikosi bora lakini kwangu ukiniambia nitakwambia nataka wachezaji saba,” alisema Kitambi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic