OKWI AKIPAMBANA NA MABEKI WA AZAM |
Kiungo Athumani Iddi
‘Chuji’ amebaki Dar es Salaam huku kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel
Okwi akiwa bado kwenye mgomo.
Yanga ipo Arusha kwa ajili ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara ambapo
ushindi ni muhimu kwao ili iendelee kuwania kutetea taji lake ambalo pia
linaweza kutua Azam ikiwa watashinda mechi ya kesho dhidi ya Mbeya City.
Mtoa taarifa kutoka klabuni hapo amesema kuwa Yondani alirejea jana
asubuhi na kujiunga kwenye msafari ulioelekea Arusha, lakini akasisitiza kuwa
benchi la ufundi halijamchukulia hatua yoyote.
Taarifa za ndani za Yanga zimeeleza kuwa Chuji ameachwa Dar kama
ilivyo kwa Okwi ambaye anaendeleza mgomo wa kutaka malipo yake.
“Ila bado anaonekana Chuji amekuwa mtovu wa nidhamu, mara kwa mara
anafanya makosa, anaomba radhi, halafu anarudia mara nyingine,” alisema.
Mgomo wa Okwi, inaelezwa anadai dola 40,000 ambazo zimebaki katika
dola 100,000 alizotakiwa kulipwa.
Hakuna kiongozi wa Yanga aliyejitokeza kulizungumzia suala hilo zaidi
ya wale wa benchi la ufundi ambao wamekuwa wakisisitiza kuwa ni suala kati ya
Okwi na uongozi.
okwi! okwi! utafikiri mchezaji kumbe galasa fulani tuu, fukuzeni hana jipya zaidi kutuletea mgogoro wana yanga, yanga ya wenyewe wenye damu za kijani,
ReplyDelete