May 9, 2014

MBOGO AKIMTHIBITI NGASSA


Baada  ya timu yake ya Rhino Rangers ya Tabora kushuka daraja, beki wa kati, Ladislaus Mbogo amesema hana mpango wa kuendelea kuichezea timu hiyo.


Rhino imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu Bara msimu uliomalizika ikiwa pamoja na JKT Oljoro na Mgambo Shooting ambazo zote zitashiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.

Mbogo ambaye ni beki wa zamani wa Toto, ameliambia gazeti hili kuwa, hivi sasa yeye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa miaka miwili aliyokuwa anaitumikia Yanga iliyompeleka kwa mkopo Rhino Rangers kumalizika.

Mbogo alisema kuwa, yupo tayari kwenda kuichezea timu yoyote itakayomhitaji kwa ajili ya msimu ujao wa 2014-2015 kwa makubaliano maalumu.

“Hivi sasa nipo nyumbani Mwanza nimepumzika tu, sitarejea tena kuichezea timu hiyo baada ya kushuka daraja, ninasubiri timu yoyote itakayonihitaji kwa ajili ya msimu ujao. Soka ni ajira inayoendesha maisha yangu,” alisema Mbogo.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic