PODAMALI AKIWA KAZINI, HAPA ANAWAFUA DIDA NA BARTHEZ |
Kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali, yupo mbioni kurekodi video
ya nyimbo zake za Domo la Mamba Haliishi Kujilamba na Sweet Mama zinazotarajiwa
kutoka hivi karibuni.
Pondamali amefunguka kuwa, kwa sasa tayari ameshazisambaza nyimbo
zake zote katika vituo mbalimbali vya redio na kudai kuwa, yupo katika hatua ya
mwisho ya kurekodi ili aweze kuzirusha.
“Nipo katika hatua za mwisho za kurekodi video za nyimbo zangu mbili
hivi karibuni na tayari nimeshasambaza audio katika vituo vya redio na
zinaendelea kupigwa. Hadi sasa nina nyimbo tano, bado tatu ili niweze kutimiza
nane niweze kupata albamu,” alisema Pondamali.
0 COMMENTS:
Post a Comment