Mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi, amesema
anaweza kuondoka na kujiunga na Stand United ya Shinyanga, kama watamhitaji.
Stand United imefanikiwa kupanda kwenye Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza na msimu wa 2014-15 itaanza kupambana na vigogo.
Bahanuzi ambaye hana nafasi ya uhakika katika
kikosi cha Yanga amesema yuko tayari kwa kuwa maisha yake ni soka.
“Wanaweza kuja tukazungumza, soka ndiyo kazi yangu
na kazi ndiyo maisha, hivyo waje tu,” alisema.
Tokea msimu uliooita, Bahanuzi amepoteza uhakika wa
namba katika kikosi cha Yanga.
Lakini misimu miwili iliyopita, alikuwa tegemeo
hasa baada ya kuisaidia Yanga kubeba Kombe la Afrika Mashariki na Kati, ikiwa
chini ya Tom Saintfiet, raia wa Ubelgiji.
0 COMMENTS:
Post a Comment