Kocha Hans van der Pluijm ameshauri Yanga kuhakikisha
inambakiza aliyekuwa msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa.
Pluijm ambaye amepata mkataba wa mwaka mmoja wa
kufundisha soka nchini Saudi Arabia, amewashauri Yanga kwamba Mkwasa ni kati ya
makocha bora na wachapakazi.
“Kocha amesema amefanya kaiz kwa muda mrefu barani
Afrika, kati ya makocha ambao amefanya nao kazi kwa uhakika ni Mkwasa.
“Amesisitiza tufanye kila linalowezekana
kuhakikisha anabaki, amesema hata akija kocha yupi, basi lazima tuhakikishe
anabaki pale,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka kutajwa.
Pea ya Mkwasa na Pluijm imeimaliza ligi kuu ikiwa
katika nafasi ya pili na tayari Yanga wameanza mchakato wa kusaka kocha mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment