Kikosi cha Barcelona kitaanza kazi ya kujiweka
safi na imara kwa ajili ya msimu ujao siku ya Julai 14.
Kocha Mkuu mpya, Luis
Enrique, ameishawatangazia wachezaji wote kufika kambini siku hiyo.
Itakuwa ni siku moja katikati baada ya Kombe la
Dunia.
Hali hiyo imeonyesha Enrique hataki utani na kazi
na kweli amepania kukiimarisha kikosi hicho.
Amesema wachezaji wote watatakiwa kufika katika Viwanja
vya 'Ciudad Deportiva Joan Gamper' ili kuanza mazoezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment