Wakati Yanga, Simba zikiendelea
kupambana kupata viongozi huku kukiwa na malumbano, Florentino Pérez, Kocha Mkuu, Carlo
Ancelotti mmoja wa Wakurugenzi, José Ángel Sánchez, wamekutana.
Watatu hao katika klabu ya watu maarufu Señorío de
Alcocer' na kufanya mkutano huo mfupi, kuwa ni nini cha kufanya msimu ujao.
Inaonekana hawajalewa na kombe hilo maarufu kama
'Décima' walilokuwa wakilitafuta kwa miaka nenda
rudi.
Badala yake wameanza mapema kutaka kujua, kocha
anataka nini, kambi iwe wapi na nini cha kufanya.
Lakini Yanga hawajajua kocha mkuu ni nani, Simba
hawajui wachezaji ni kina nani na kocha Zdravko Logarusic atarudi au la.
0 COMMENTS:
Post a Comment