Tanzania inaendelea kufanya vizuri kwenye Michezo ya Afrika kwa
Vijana (AYG) kwa upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka
15 baada ya leo (Mei 23 mwaka huu) baada ya kuwachapa wenyeji Botswana mabao
2-0.
Mabao ya Tanzania katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa SSKB
jijini Gaborone yalifungwa na David Uromi dakika ya sita huku Anthony Amede
akitupia la pili dakika ya 46.
Katika mechi yake ya kwanza, Tanzania ilitoka sare ya bao 1-1 na
Mali ambapo michezo hiyo inaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha
SuperSport cha Afrika Kusini.
Tanzania itacheza mechi yake ya tatu keshokutwa (Mei 25 mwaka
huu) dhidi ya Swaziland, itakuwa tena uwanjani Mei 27 mwaka huu kuikabili
Nigeria wakati mechi ya mwisho itafanyika Mei 29 mwaka huu dhidi ya Afrika
Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment