Kocha Hans van Der Pluijm wa Yanga anaondoka leo
kwenda Saudi Arabia kusaini mkataba mpya.
Anakwenda kuingia mkataba na timu ya Ligi Kuu ya Shoala FC ambayo imevutiwa naye.
Pluijm amepata timu ya kuifundisha nchini Saudi Arabia.
Pluijm amepata timu ya kuifundisha nchini Saudi Arabia.
Pluijm ameiambia SALEHJEMBE kuwa ofa kubwa ndiyo
inamuondoa Yanga.
“Ofa ni kubwa sana, yoyote asingevumilia na
nimezungumza na viongozi wa Yanga, wamekubaliana na hilo.
“Naondoka kwenda Saudi Arabia, baada ya kusaini
mkataba nitarudi hapa na kuisaidia Yanga kupata wachezaji,” alisema.
Pluijm ameinoa Yanga kwa nusu msimu na kuiwezesha
kushika nafasi ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment