Kocha Zdravko Logarusic amewasilisha ripoti yake ya
mwisho wa msimu inayoagiza kutemwa kwa wachezaji wote Simba na kubaki 13 tu wa
kikosi cha kwanza.
Logarusic ambaye yuko kwao Croatia kwa mapumziko
ametema wachezaji wote na kutaka 13 ndiyo wabaki na maramoja usajili uanze.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zinaeleza
ripoti hiyo tayari iko mikononi mwa kamati ya usajili inaoongozwa na Zacharia
Hans Pope.
Akizungumza jana kutoka Croatia, Logarusic
alikubali kuwa ametema idadi kubwa ya wachezaji lakini akasisitiza hawezi
kuianika ripoti yake hadharani.
“Viongozi wanajua, ninataka kusuka kikosi upya na
kweli wengi nimependekeza waachwe,” alisema.
Majina ya aliotaka wabaki, yaani wachezaji 13
anaoamini bado wana sifa ya kucheza Simba, ni hawa:
Ivo
Mapunda, Rashid Issa ‘Baba Ubaya’, Donald Musoti, William Lucian, Said Ndemla,
Nassor Said ‘Chollo’, Amri Kiemba, Jona Mkude, Abdallah Seseme, Haruna
Chanongo, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amissi Tambwe na Awadhi Juma.
0 COMMENTS:
Post a Comment