Hali si shwari kwa mara nyingine ndani ya Klabu ya Coastal Union ya Tanga
kutokana na msuguano wa viongozi, sasa limeibuka lingine jipya.
Makamu Mwenyekiti wa Coastal, Steven Mnguto amedai kuwa anamshangaa
mwenyekiti wake, Ahmed Aurora kuwachajisha shilingi 10,000 mashabiki wanaotaka
kuchukua fomu za kujiunga na uanachama wa klabu hiyo kwa kuwa siyo sahihi na
kudai kuwa kiwango sahihi ni shilingi 1,000.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mnguto alisema migogoro imekuwa mingi
klabuni hapo na imechangia kuivuruga timu huku akidai kuwa suala hilo la
wanachama lipo wazi tangu siku nyingi.
“Hili suala la fomu linanichanganya, miaka mingi utaratibu wetu ni wa
kutoa elfu moja, sasa huyu mwenyekiti hiyo ada ya elfu kumi ameitoa wapi!”
alisema Mnguto.
Alipotafutwa Aurora hakuweza kupatikana kulizungumzia suala hilo hadi
gazeti hili linaingia mitamboni..
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment