Katika kuhakikisha kikosi chao kinaimarika
vyema kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, Kipa namba wa Simba, Ivo Mapunda,
ameutaka uongozi wa timu hiyo kuhakikisha unafanya usajili wao kwa kupitia
ripoti ya kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic.
Ivo alisema
kuwa timu yao kocha ndiye anayejua upungufu katika kikosi chake, hivyo ili timu
ifanye vizuri basi lazima usajili ufanywe na yeye.
Alisema kuwa, katika kikosi chao sehemu
nyingi zilikuwa na upungufu ambao unahitajika kuboreshwa katika kukiimarisha
zaidi ili ubingwa wa msimu ujao wauchukue wao.
“Siku zote usajili unafanywa na kocha na
siyo viongozi wa timu, hivyo katika kuhakikisha kikosi chetu kinaimarika zaidi
basi ripoti ya usajili aliyoiacha kocha ndiyo ifanye usajili.
“Zipo sehemu nyingi nilizoziona katika msimu
uliopita ambazo zinahitaji kuboreshwa, ikiwemo kuiboresha safu ya ulinzi kwa
kuanza na mabeki wote watatu wa pembeni namba mbili na tatu,” alisema Ivo na
kuongeza:
“Pia wanahitajika viungo, washambuliaji na
mawinga wenye uwezo na uzoefu mkubwa wa kucheza soka ili na sisi msimu ujao
tufanye vizuri ikiwemo kuchukua ubingwa, tushiriki michuano ya kimataifa baada
ya kukosa ya mwakani.”
0 COMMENTS:
Post a Comment