PONDAMALI (KATIKATI) AKIWAFUA MAKIPA WA YANGA, DIDA NA BARTHEZ |
Hauna haja ya kuona ni ajabu, lakini ndiyo uamuzi wa Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali, amesema mara baada ya
kumaliza mkataba wake na Wanajangwani, atastaafu soka.
Atakapostaafu atafanya kazi ipi? Pondamali anasema anayo, anaijua nayo ni masumbwi!
Pondamali amesema hana mpango
wa kuendelea tena kufundisha soka kwa kuwa umri unaenda, hivyo atageukia katika
masuala ya kibiashara pamoja na kuwa muandaaji wa michezo ya ngumi za kulipwa
hapa nchini.
“Mimi ni ‘coordinator’ wa ngumi ambapo kuna mwenzangu tunatarajia
kushirikiana naye, tayari tumeshapata ‘document’ zote zinazohusiana na masuala
ya kuandaa ngumi.
“Kwa sasa nimeandika ‘proposal’ na kupeleka katika kampuni
mbalimbali ili niweze kukubaliwa na kufikia tamati kwani kila kitu kinakwenda
sawa na iwapo nitafanikiwa basi nitajiingiza kwenye ngumi rasmi.
“Sina mpango wa kuongeza mkataba mwingine Yanga, wala kusaini timu
yoyote ya ligi kuu, naona ni bora niachane na masuala ya mpira baada ya
kumaliza mkataba wangu.
“Nimekuwa kipa wa timu ya taifa kwa muda wa miaka 10 na kocha wa
makipa timu ya taifa kwa muda wa miaka saba, tangu enzi za Maximo na timu
tofautitofauti na sasa nipo Yanga, hivyo naona inanitosha.
“Natarajia kwenda kukaa Tanga Handeni ambako ndiko nilipozaliwa
ili niweze kuendeleza biashara zangu pamoja na mambo ya ngumi,” alisema
Pondamali.
0 COMMENTS:
Post a Comment