KABURU |
Mchezaji wa zamani wa
Simba, Ather Mambeta mwenye kadi namba 01005 ameweka pingamizi kwa Geofrey
Nyange ‘Kaburu’.
Mambeta ameweka
pingamizi hilo kwa Kaburu aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Simba katika
utawala unaomaliza muda wake.
Amesema pingamizi
lake ni kutokana na Kaburu kujiuzulu alipokuwa madarakani, lakini akagombea
kabla ya miaka mitatu kwisha.
Pia amemumuweka
pingamizi Swed Nkwabi anayepambana na Kaburu.
Amesema Nkwabi pia
alikiuka katiba kuungana na wenzake wa kamati ya utendaji kumpindua mwenyekiti,
Ismail Aden Rage.
0 COMMENTS:
Post a Comment