Luis Enrique ndiye kocha moya wa Barcelona,
anachukua nafasi ya Tata Martino.
Enrique mwenye umri wa miaka 44, kiungo wa
zamani wa Barcelona alikuwa akiinoa Celta Vigo.
Enrique atasaini mkataba wa miaka miwili ikiwa
ni baada ya Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona, Andoni Zubizarreta kuweka wazi
kuwa Enrique, ndiye chaguo la kwanza.
Pamoja na Enrique, Barcelona imemuajiri
kocha mpya wa makipa, Marc-Andre Ter Stegen kutoka Borussia Monchengladbach ya
Ujerumani.
Enrique aliichezea Barcelona tokea mwaka 1996
hadi 2004 baada ya kujiunga nayo akitokea kwa wapinzani wakubwa wa Barca, Real
Madrid.
0 COMMENTS:
Post a Comment