Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linaandaa utaratibu utakaowawezesha washabiki kwenda jijini
Harare, Zimbabwe kushuhudia mechi ya Taifa Stars.
Mechi hiyo ya marudiano ya
Kombe la Afrika kwa ajili ya fainali zitakazochezwa Morocco mwakani itafanyika
Jumapili (Juni 1 mwaka huu) jijini Harare.
Taifa Stars inayodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager ilishinda mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0.
Usafiri huo utakuwa wa basi
ambapo washabiki wanatarajiwa kuondoka siku ya Ijumaa na kuwasili Jumapili
mchana jijini Harare ambapo watashuhudia mechi na kuanza safari ya kurejea Dar
es Salaam siku hiyo hiyo.
Washabiki wanatakiwa kuwa na
hati za kusafiria (pasipoti), nauli ya kwenda na kurudi itakuwa sh. 300,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment