Manchester City wamemaliza ule ubishi wa
nani atakuwa bingwa wa Ligi Kuu England.
Jibu limepatikana na ubingwa umekwenda
Manchester badala ya Liverpool.
Maana yake, Man City wamechukua ubingwa
huo mara mbili ndani ya misimu mitatu, mara ya mwisho walikuwa mabingwa msimu we
2011-12.
Msimu uliofuata wa 2012-13, majirani zao
Manchester United wakalibeba lakini msimu huu wakawa nyanya na City wameendelea
kulibakiza jijini Manchester.
City imebeba kombe hilo baada ya
kuitwanga West Ham kwa mabao 2-0 huku Liverpool nao wakishinda kwa 2-1 dhidi ya
Newcastle lakini ndiyo hivyo wamechukua nafasi ya pili.
Mabao ya City yalifungwa na Samir Nasri
na nahodha Vincent Kompany wakati Liverpool walianza kwa Skirtel kujifunga
kabla ya Daniel Agger na Daniel Sturridge kusawazisha na kuongeza.
Liverpool wameshindwa kuifikia City kwa
pointi mbili, walichokuwa wanaomba leo ni City kupoteza na wao washinde, lakini
ndiyo hivyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment