Mechi ya kwanza ya
raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini
Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (Mighty Warriors) itafanyika
Jumapili (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali mechi hiyo
tulipanga ichezwe Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa nia ya kuhakikisha mikoa
yote ya Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mechi za kimataifa.
Ili Uwanja wa Sokoine
uweze kuchezwa mechi za kimataifa za mashindano, Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) lilituma Mkaguzi (inspector) wake kwenye uwanja huo Jumamosi (Mei
10 mwaka huu) ambapo imeamua kuwa marekebisho yanayofanyika hayatamalizika
katika muda stahili, hivyo mchezo huo kutochezwa Sokoine.
Tunatoa mwito kwa
wamiliki wote wa viwanja kuwasiliana na TFF ili Idara ya Ufundi iwaelekeze
maboresho ya kufanya ili viwanja vingi iwezekanavyo viweze kukidhi viwango
vinavyotakiwa na CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Taifa Stars ambayo ilikuwa
kambini mkoani Mbeya itarejea Dar es Salaam keshokutwa (Mei 14 mwaka huu)
kujiandaa kwa mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment