Kitendo cha
maofisa wa Taasisisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru),
kuvamia usaili wa nafasi mbalimbali za uongozi Simba, kimewashtua wagombea wa
timu hiyo.
Tukio hilo la
maofisa hao kuvamia usaili huo wa uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Polisi
Oficer’s Mess uliopo Masaki jijini Dar es Salaam lilitokea hivi karibuni.
Maofisa hao
wawili walifika hapo majira ya saa 6:15 na kuondoka saa 6:49 mchana na
kuangalia mazingira ya hapo kabla ya baadaye kuingia kwenye ukumbi maalum
uliotengwa kwa ajili ya usaili ili kuchunguza baadhi ya mambo na baadaye
kuondoka na nyaraka na namba za simu za wagombea.
Ujio huo wa
maofisa hao uliwashtua wagombea hao na kusababisha kuanza kuhoji sababu ya
Takukuru hao kufika na kusitisha kwa muda zoezi hilo la usaili lililokuwa
linaendelea kwa upande wa wajumbe baada ya kumaliza nafasi ya rais na makamu
wake.
“Kipi kimewaleta
hapa Takukuru, kuna nini kinachoendelea kwani, mbona amani na usalama upo wa
kutosha? Wao walitakiwa wasubirie tumalizie usaili kwanza, hayo mengine yafuate
baadaye,” alisikika mmoja wa wagombea hao.
0 COMMENTS:
Post a Comment