Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali, amesema hakuna asiyejua kwamba yeye na
mgombea wa nafasi ya urais wa Simba, Evans Aveva ni damudamu.
Dalali amesema yeye ni mchapakazi kama ilivyo kwa Avev, hivyo ni lahisi kuwa watu wawili wanaoelewana.
Lakini akaongeza, Aveva ni mtu anayeipenda Simba kwa dhati na si maslahi, hivyo lazima atakuwa ni rafiki yake kwa kuwa naye ni mtu anayeipenda Simba na maendeleo yake na si kupata maslahi kupitia klabu hiyo.

Simba
inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu Juni 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam
iwapo hakutatokea mabadiliko yoyote kufuatia mgombea wa nafasi ya urais
aliyeenguliwa, Michael Richard Wambura kukata rufaa TFF.
Dalali alisema hawezi kuzungumza kitu chochote kuhusu
kuenguliwa kwa Wambura na kudai kuwa, yeye anajulikana wazi kuwa ni mfuasi wa
Aveva ambaye ndiye anayemhitaji kuingia madarakani.
“Hakuna
kificho kuwa mimi nipo wapi, kila mtu anajua kuwa mimi ni mfuasi wa Aveva,
hivyo siwezi kuzungumzia kitu chochote juu ya kuenguliwa kwa Wambura.”
0 COMMENTS:
Post a Comment