Tanzania imeendelea kung’ang’ara
kwenye Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) kwa upande wa mpira wa miguu kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya jana (Mei 25 mwaka huu) kuichapa
Swaziland mabao 3-0.
Mabao ya Tanzania katika
mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Gaborone, Botswana yalifungwa na
Amani Ally dakika ya sita, Nasson Chanuka dakika ya 32 wakati Amos Kennedy
alikamilisha ushindi huo kwa bao la dakika ya 53.
Katika mechi yake ya kwanza,
Tanzania ilitoka sare ya bao 1-1 na Mali na baadaye kuwafunga wenyeji Botswana
mabao 2-0. Mechi za michuano hiyo zinaoneshwa moja kwa moja na kituo cha
televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini.
Tanzania itacheza mechi yake ya nne kesho (Mei 27 mwaka huu)
dhidi ya Nigeria wakati mechi ya mwisho itafanyika
Mei 29 mwaka huu dhidi ya Afrika Kusini.
IMENDIKWA NA BONIFACE WAMBURA, MSEMAJI TFF
Mei 29 mwaka huu dhidi ya Afrika Kusini.
IMENDIKWA NA BONIFACE WAMBURA, MSEMAJI TFF
0 COMMENTS:
Post a Comment