Kocha
a ukocha wa mpira wa miguu kwa ajili ya Leseni A na B zinazotambuliwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) zitafanyika jijini Dar es
Salaam kuanzia Juni 2 mwaka huu.
Ada
kwa kozi ya Leseni A itakayoanza Julai 21 hadi 26 mwaka huu ni sh. 300,000
wakati ile ya Leseni B itakayofanyika kuanzia Juni 2 hadi 15 mwaka huu ni sh.
200,000. Maombi ya kushiriki kozi hizo yatumwe kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati kwa upande wa Zanzibar yatumwe kwa Katibu
Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kabla ya Mei 31 mwaka huu.
Washiriki
ambao watajitegemea kwa chakula watalipa ada hizo wakati wa usajili
utakaofanyika Juni 1 mwaka huu kwa upande wa Leseni B na Leseni A watalipa
Julai 20 mwaka huu vilevile wakati wa usajili.
TFF itatoa malazi kwa
washiriki kwenye hoteli yake iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati
wakufunzi wa kozi hizo ni Sunday Kayuni na Salum Madadi ambao wanatambuliwa na
CAF. Pia CAF baadaye itatuma Mkufunzi atakayetunga na kusimamia mitihani hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment