Kutokana na tukio lililotokea jana (Aprili 30 mwaka huu) kwenye
kambi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya likihusisha
usajili wa baadhi ya timu, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo mzima wa tukio
hilo.
Baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF
kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua.
TFF inatoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu
kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao.
Domayo amesajiliwa na Azam FC akiwa kambini Taifa Stars mjini Tukuyu wakati timu hiyo inajiandaa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi.
Usajili wake umezua gumzo huku TFF ikiendelea kusisitiza kwenye kambi za timu ya taifa si sehemu sahihi ya kufanya masuala ya usajili.
Hap malinzi amechemsha anataka alete unazi wake wa yanga kwani juna ajabu gani hapo ? Au kunya anye kuku akinya bata kaharisha? Tumeshuhudia Yanga ikimtorosha kelvin yondani wakati yupo kambini na timu ya taifa wakamtorosha wakamsajil wakat huo akiwa ni mchezaj wa simba, na hapo haikutosha wakamtorosha huyo Domayo wakamsainisha wakati huo alikuwa ni mchezaj wa Jkt, Simba nao wakamtorosha kiemba wakampa mkataba mpya wakat yupo kambini, lkn leo kafanya Azam ni kosa la kutafutwa wakili alichunguze, haki ipo wapi hapo?
ReplyDeleteKwahiyo aendeleze makosa yaliyokuwa yakifanywa siku za nyuma? kweli tunasafari ndefu sana kuyafikia mafanikio kwani mmeridhika na hali mliyonayo!
Delete