June 22, 2014



Kombe la Dunia lina mambo yake, angalia ndugu hawa wawili walivyochuana uwanjani wakitaka mataifa mawili yaibuke na ushindi kila mmoja akivutia kwake.

Kaka wa damu kutoka familia ya Boateng Jerome na Kevin-Prince walipambana mmoja akitaka Ghana ishinde na mwingine Ujerumani, katika hatua ya makundi.

Hii ni mara ya pili Ghana na Ujerumani kukutana kwenye Kombe la Dunia na Jerome akikipiga Ujerumani, ndugu yake akiichezea Ghana.
Wawili hao wazazi wao, mmoja anatokea Ujerumani na mwingine Ghana na kila mmoja kachagua kucheza upande anaovutiwa nao.

Wote wamezaliwa jijini Berlin, mji mkubwa zaidi kuliko yote nchini Ujerumani baba akiwa mwenye asili ya Ghana.
Jerome ambaye ni beki wa mabingwa wa Ujerumani akaamua kuichezea Ujerumani na kutoka Schalke, Kevin-Prince yeye akasema ataiwakilisha Ghana.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic