Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) ukiongozwa na Jamal Malinzi jana (Juni 21 mwaka huu) mjini
Dodoma umekutana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii chini ya
Mwenyekiti wake Mheshimiwa Said Mtanda (Mbunge wa Mchunga).
Katika kikao hicho TFF ilielezea mikakati yake ya
maendeleo ya mpira wa miguu pamoja na maandalizi ya timu ya Taifa kwa ajili ya
mchezo wake dhidi ya Msumbiji.
TFF iliiahidi Kamati ya Bunge kuwa itaendelea kuwa
inafanya shughuli zake kwa karibu na Serikali na kamati hiyo ya Bunge.
Katika kikao hicho, ujumbe wa benki ya CRDB ukiongozwa
na Meneja wa Electronic Banking, Bw. Mangire Kibanda ulihudhuria ili kutoa
ufafanuzi juu ya mradi wa kuuza tiketi za elektroniki, mradi ambao maandalizi
yanaendelea vizuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment