June 2, 2014



Mshambuliaji mkongwe David Villa amejiunga na New York City FC ya Marekani ambayo amesaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea.


Villa ameiacha Atletico Madrid siku chache baada ya kulikosa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushindwa kuizuia Real Madrid ndani ya sekunde 90 tu.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 32 amemshukuru aliyekuwa kocha wake, Diego Simeone kwa kuonyesha kuendelea kumhitaji kwa kuwa alimshawishi abaki.
Pamoja na kukosa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini katika msimu wake wa kwanza na mwisho na Atletico aliiisaida kutwaa ubingwa wa La Liga.
Kabla ya kutua Atletico, Villa alikuwa mshambuliaji nyota wa Barcelona ya Hispania pia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic