Maziko ya
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati huo
likiitwa FAT, Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe yanafanyika leo (Juni 10
mwaka huu) Magugu, Babati mkoani Manyara.
Kanali Mwanakatwe
alifariki dunia Juni 7 mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo
jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu baada ya kuanguka bafuni
nyumbani kwake Mbezi Beach.
TFF imetoa ubani wa sh. laki tano kwa
familia ya marehemu Kanali Mwanakatwe, na katika maziko hayo inawakilishwa na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Kanda ya Arusha na Manyara, Omari Walii.
0 COMMENTS:
Post a Comment