Kozi ya makocha wa mpira wa
miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
iliyodumu kwa wiki mbili inafungwa kesho (Juni 20 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
Makocha 26 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wameshiriki katika
kozi hiyo chini ya wakufunzi wa CAF, Sunday Kayuni, Salum Madadi wa Tanzania na
Honory Janza kutoka Zambia. Ufungaji wa kozi hiyo unatarajiwa kufanywa saa 5
asubuhi kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Walioshiriki kozi hiyo ni Abdalla Mohammed Juma (Zanzibar),
Abdul Banyai (Temeke), Abdul Nyumba (Temeke), Abdulmutik Haji (Zanzibar), Aley
Mohammed (Zanzibar), Ali Vuai Shein (Zanzibar), Dennis Kitambi (Morogoro),
Dismas Haonga (Ilala), Emmanuel Massawe (Shinyanga), Fikiri Elias (Arusha),
Fulgence Novatus (Mwanza), Hababuu Ali Omar (Zanzibar), Juma Mgunda (Tanga) na
Kidao Wilfred (Ilala).
Wengine ni Maka Mwalwisi
(Mbeya), Malale Hamsini Keya (Zanzibar), Mecky Maxime (Morogoro), Mohammed
Tajdin (Temeke), Mussa Furutuni (Dodoma), Nassor Salum Mohamed (Zanzibar),
Peter Mhina (Ruvuma), Said Mohamed Abdulla (Zanzibar), Salim Makame (Zanzibar),
Salum Ali Haji (Zanzibar), Sebastian Nkoma (Ilala), Wane Mkisi (Dar es Salaam).
0 COMMENTS:
Post a Comment