Kikosi cha timu ya soka ya taifa, Taifa Stars
kimesonga mbele na itakutana na Msumbiji katika hatua ya mwisho kuwania kucheza
makundi ya Kombe la Mataifa Afrika nchini Morocco, mwakani.
makundi ya Kombe la Mataifa Afrika nchini Morocco, mwakani.
Msumbiji imesonga mbele kwa kuwang'oa Sudan Kusini na sasa ni zamu ya kuwavaa Stars.
Stars imewang’oa Zimbabwe baada ya mechi iliyomalizika hivi punde mjini Harare kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Stars imewang’oa Zimbabwe baada ya mechi iliyomalizika hivi punde mjini Harare kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Stars
ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na John Bocco.
Lakini katika mechi ya leo, kazi haikuwa lelemama
baada ya wenyeji Zimbabwe kupata bao mapema katika dakika ya 12 kupitia kwa
Danny Phiri.
Lakini Stars chini ya Mart Nooij ikasawazisha
katika dakika ya dakika ya 26 kupitia Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Kipindi cha pili kiliponza tu, Thomas Ulimwengu
akaongeza la pili katika dakika ya 46 na dakika ta 55, Willard Katsande
akaisawazishia Zimbabwe.
Pamoja na juhudi za mwamuzi wa mchezo huo kuongeza
dakika 7 za nyongeza, lakini bado mambo yalikuwa magumu kwa wenyeji na matokeo
hayakubadilika.
Hivyo Stars imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2
na inasubiri makundi sasa.
Timu nyingine za Afirka Mashariki zimesonga mbele
ambazo ni Kenya, Uganda na Rwanda ambayo iliitungua Libya kwa mabao 3-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment