Mashabiki wa Atletico Madrid wameanzsiha bonge la
kampeni kupitia mitandao mbalimbali wakipiga klabu yao kutaka kumsajili,
Roberto Soldado.
Mashabiki hao wameonyesha kulaani wazi kwamba
Soldado ni kimeo na ameshindwa kung’ara licha ya Tottenham kumwaga pauni
milioni 26 kumnasa.
Atletico wameanza kumpigia hesabu Soldado baada ya
David Villa kuamua kwenda kucheza soka nchini Marekani.
Kutokana na kutofanya vizuri kwa kufunga mabao sita
tu, ameachwa katika kikosi cha Hispania kinashoriki Kombe la Dunia.
Mashabiki hao wa atletico ambao ndiyo mabingwa wa
La Liga wamesema hawana shida na Soldado huku wakiuasa uongozi usimsajili.
Hata hivyo baadhi ya timu kama Inter Milan ya
Italia, zimeonyesha kuwa na nia ya kumpata mshambuliaji huyo.
Pamoja na yote, kumekuwa na taarifa nyingine kwamba
Soldado atabaki White Heart Lane kutokana na matumaini ya ujio wa kocha mpya akiamini
atamsaidia.
0 COMMENTS:
Post a Comment