Kocha wa wa Azam FC,
Joseph Marius Omog amerejea nchini akiongozana na mshambuliaji mpya wa kikosi hicho
cha mabingwa wa Tanzania Bara.
Mshambuliaji huyo mpya
kutoka Mali, anaitwa Ismail Diarra na ataanza kazi pamoja na Omog, keshokutwa.
Diarra ameingia mkataba wa miaka miwili kuichezea Azam FC ambayo kwa miaka miwili mfululizo imeshiriki michuano ya kimataifa chini ya Caf.
Msemaji wa Azam FC,
Jaffar Idd amesema wawili hao watakuwa na siku mbili za kupumzika ambazo ni leo
na kesho.
Omog raia wa Cameroon
ndiye aliipa Azam FC ubingwa kwa mara ya kwanza tokea ianze kushiriki Ligi Kuu
Bara.
“Kweli kocha
awalisili leo akiwa na mshambuliaji huyo na wataanza kazi Jumatatu.
“Kama unavyojua,
wachezaji wengine wa Azam walianza mazoezi pamoja,” alisema Jaffar.
Wachezaji wengine wa
Azam FC ambayo itaiwakilisha Tanzania katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika
walianza mazoezi takribani wiki moja kabla.
0 COMMENTS:
Post a Comment