June 10, 2014



Kocha asiyeisha vituko, Jose Mourinho amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema alipata ajira ya kuinoa timu ya taifa ya England, lakini mkewe akamkataza.


Mourinho raia wa Ureno amesema alifanya mazungumzo na Shirikisho la Soka England (FA) na kukubaliana nao kila kitu mwaka 2007, lakini kabla ya kuanza kazi, mkewe akapinga hilo lakini kwa ushauri.

Bosi huyo wa Chelsea amesema, tayari mkataba ulikuwa mezani, tayari kwa ajili ya kusainiwa lakini Matilde ambaye ndiye mkewe akamuonya.
Mourinho amesisitiza kwamba pamoja na kuikosa nafasi hiyo ambayo ilichukuliwa na Steve McClaren, kamwe hajawahi kujuta.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic