Wachezaji wa
Tanzania walioko Uholanzi, Dickson Ambundo na Shiza Yahya wameanza kuonekana
muda na waandaaji ya mashindano ya AEGON Copa Amsterdam.
Kwa mujibu wa
wakala wa wachezaji wa Uholanzi, Denis Kadito, AEGON Copa Amsterdam ni
mashindano ya kimataifa yanayoshirikisha timu kubwa kutoka nchi mbalimbali
ulimwenguni kwa wachezaji wa miaka chini ya 19.
Kwa Uholanzi, Ajax
Amsterdam huwa lazima washiriki, na pia huwa kuna timu ya ridhaa
inayotengenezwa kwa kuchagua “best talent” kutoka Uholanzi. Mchujo wa wachezaji
hao kutengeneza timu ya kombaini, ulianza na wachezaji wasiopungua 1,000.
Kombaini hiyo
inaitwa Men United na inafundishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa
Uholanzi, Ronald de Boer. Ronald e Boer ni pacha wa kocha wa Ajax (First team).
Ronald de Boer pia
ni kocha wa wachezaji washambuliaji wa Ajax. Shiza na Ambundo waliingizwa
kwenye mchujo na wakafanya vizuri, mwishoni wakaitwa kwenye timu ya wachezaji
18 waliotengeneza timu ya Men United. Hii ni mara ya kwanza wachezaji wasio
Waholanzi kuingizwa katika timu hiyo.
Mashindano ya Copa
Amsterdam yameanza juzi (Juni 8 mwaka huu) na yanaisha kesho (Juni 11 mwaka
huu. Katika mashindano hayo kuna makundi mawili. Kundi A ni AFC Ajax
(Amsterdam), Ajax Cape Town ( Afrika Kusini), Fluminense (Brazil), Hamburg SV
(Ujerumani) wakati B ni Men United, Panathinaikos (Ugiriki), FC Aerbin (China)
na Cruizero (Brazil).
Shiza na Ambundo wamecheza mechi zote tatu.
Shiza amekuwa akicheza namba tatu wakati Ambundo anapiga namba tisa, saba na
kumi na moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment