Kiungo nyota wa UiTM FC, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini
Malaysia, Mtanzania, Abdi Kassim ‘Babi’, amesema tatizo ambalo linawafanya
wachezaji wa Kibongo washindwe kucheza soka la kulipwa ni kukosekana kwa chips
mayai sehemu ambazo wanatakiwa kwenda kucheza.
Babi ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja, amepata mafanikio ya
kupewa unahodha kwa muda mfupi tangu alipojiunga na kikosi hicho mapema mwaka huu.
Akizungumza na SALEHJEMBE moja kwa moja kutoka Malaysia,
Babi alisema anashangazwa na kitendo cha wachezaji wa Kibongo kukataa ofa za
kucheza soka la kulipwa na anahisi labda tatizo kubwa ni huko waendako hakuna
chips mayai, hali inayosababisha waamue kukataa kwa kuwa wamezoea chakula hicho.
Alisema mtu mwenye malengo siku zote hawezi kushindwa kuyatafuta
lakini anawashangaa wachezaji wengi wa Kibongo jinsi wanavyolichukulia soka.
“Inawezekana wakawa ‘wanamis’ chips mayai wanapokuwa nje ya Bongo
au familia lakini mtu mwenye malengo hawezi kushindwa, mimi huku nacheza vizuri
na wala hakuna hizo chips,” alisema Babi na kuongeza:
“Soka la huku lina ushindani mkubwa sana, tena kuliko hata la huko
Bongo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment