June 2, 2014



Mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba, ameamua kuachana na ukapera baada ya hivi karibuni kufunga pingu za maisha na mzazi mwenziye, anayejulikana kwa jina la mama Genevieve.


Mwaikimba alikuwa akiishi na mzazi mweziye huyo bila kufunga pingu za maisha hadi alipoamua kufanya hivyo Mei 17.

Akizungumza na Championi Jumatatu, mdogo wa bibi harusi, Laula Willbard, amefunguka kuwa mshambuliaji huyo alifunga ndoa hiyo katika Kitongoji cha Ipinda wilayani Kyela, Mbeya.
“Mwaikimba amefunga ndoa Mei 17 kwa kumuoa mzazi mweziye Rukia (Mary) Ally Seif katika Kanisa la KKKT ambapo Send Off yake ilifanyika Mei 10 katika Ukumbi wa Mwika Hall jijini Dar.
“Sherehe hiyo ilihudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wachache tu bila kuwa na viongozi wa timu yake, nadhani mwenyewe hakutaka kuwafahamisha watu juu ya suala hili lakini harusi yake ilifana sana,” alisema Laula.
Mchezaji mwenzake na Mwaikimba katika kikosi cha Azam FC, beki Aggrey Morris, amempongeza straika huyo kwa hatua aliyoifikia ya kuuaga ukapera kwa kufunga pingu za maisha jijini Mbeya.
Kwa upande wa Mwaikimba alipopigiwa simu kutakiwa kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo, simu yake iliita bila kupokelewa, hali iliyotafsiriwa kuwa pengine bado yupo ‘honeymoon’.
 SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic