June 4, 2014

MUSOTI (KUSHOTO) AKIWA MAZOEZINI SIMBA, MSIMU ULIOPITA.


Beki kisiki wa kati wa Simba SC, Mkenya, Donald Musoti ameanza kujifua mapema zaidi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 24, mwaka huu.


Akizungumza moja kwa moja kutokea Nairobi, Kenya, Musoti ambaye ni beki wa zamani wa Gor Mahia ya nchini humo, amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuridhika na mapumziko aliyoyapata tangu aliporudi kwao baada ya kumalizika kwa ligi, Mei 19, mwaka huu.

“Mimi ni mchezaji na haipendezi nikatumia muda wa likizo kwa kukaa tu bila ya kujifua kidogo, kwa hiyo wiki mbili zilizopita nilikuwa nakimbia barabarani pamoja na mazoezi mengine binafsi ya kujenga stamina.
“Ila kuanzia Jumatatu (juzi) nitaanza rasmi kuingia ‘ground’ na kufanya mazoezi ya kisoka zaidi, unajua ni vizuri nikianza mapema kwa sababu ligi haipo mbali sana,” alisema Musoti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic