June 8, 2014



Daniel Sturridge ndiye alipoteza nafasi muhimu ya England kuifunga Honduras katika mechi yake ya mwisho ya kirafiki kabla ya kwenda kuivaa Italia, Jumamosi ijayo.


Lakini naye akanusurika kujeruhiwa vibaya baada ya shabiki kurusha kopo la bia aina ya Heineken ambalo lilimkosa sentimeta chache.
Kama lingempata, hakika mshambuliaji huyo wa Liverpool angekuwa matatizoni na huenda angelazimika kupata matibabu hispitalini.
Hata hivyo, haikujulikana shabiki yupi alirusha kopo hilo kutoka jukwaani wakati England ikitika sare bila ya kufungana dhidi ya Honduras mjini Miami, Marekani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic